Hatua Za Msanii Kujisajili

📅 August 11, 2026 • Updated: August 11, 2026
Kabla ya Kuanza Hakikisha una vitu hivi: 📧 Barua pepe inayotumika 📱 Namba ya simu (itakayotumiwa kwa malipo) 🆔 Namba ya NIDA 📸 Picha ya Kitambulisho (NIDA au Pasipoti) 🤳 Selfie (picha ya sura yako mwenyewe) 📄 Barua ya Mchungaji/Padre (Kwa Group tu) Hatua ya 1: Taarifa za Akaunti Barua Pepe - Andika barua pepe yako Jina Kamili - Jina lako halisi Namba ya Simu - Mfano: 0719364924 Aina ya Akaunti - Chagua: => Single Artist - Msanii binafsi => Choir / Group - Kwaya au kikundi Nenosiri - Weka nenosiri (angalau herufi 4) Thibitisha Nenosiri - Andika tena Hatua ya 2: Taarifa za Msanii / Kwaya Jina la Jukwaa - Jina la msanii au kwaya yako Namba ya NIDA - Namba yako ya kitambulisho Mwaka wa Kuanzishwa - Mwaka ulioanzisha (hiari) Mtu wa Kuwasiliana - Jina la mwasiliani Namba ya Mwasiliani - Namba ya simu Anwani - Anwani yako halisi Nchi - Chagua Tanzania Mkoa - Chagua mkoa ulipo Wilaya - Andika wilaya yako (hiari) Hatua ya 3: Malipo na Nyaraka A. Taarifa za Mobile Money Namba ya Mobile Money - Namba iliyosajiliwa M-Pesa/Tigo Pesa/Airtel na iwe imesajiliwa na kitambulisho cha NIDA ulichokitumia kujisajili. Mtoa Huduma - Chagua Vodacom, Tigo, Airtel, au Halotel B. Nyaraka za Uthibitisho Kwa SINGLE ARTIST: Pakia picha ya NIDA >> Pakia selfie yako Kwa CHOIR / GROUP: >> Pakia picha ya NIDA ya mwenyekiti Pakia barua ya mchungaji/padre C. Viongozi (Kwa Group tu) Jaza taarifa za viongozi wengine wawili: Jina Kamili Namba ya Simu Barua Pepe Zao D. Makubaliano Kubali Masharti na Sheria Kubali Sera ya Faragha na usiome. Baada ya Usajili - Utapokea barua pepe ya kukaribisha - Mkataba utaambatanishwa kwenye barua pepe - Pakua mkataba, usaini, na upakie tena - Subiri uthibitisho (saa 24-48) - Akaunti yako itahakikiwa na itawekwa live. Maswali Yanayoulizwa Sana 1. Je, usajili ni wa bure? Ndiyo, usajili ni bure kabisa. 2. Je, nahitaji kuwa na NIDA? Ndiyo, NIDA inahitajika kwa uthibitisho. 3. Je, ninaweza kujiunga kama group? Ndiyo, kwaya na vikundi vyote vinakaribishwa. 4. Je, malipo yanafanywaje? Malipo yanatumwa kwa mobile money yako ndani ya dakika chache. 5. Je, uthibitisho unachukua muda gani? Saa 24 hadi 48 baada ya kupakia mkataba.