Namna Ya Kupakia Album / Ep
📅 August 10, 2026
• Updated: August 11, 2026
• Has Video
Unataka kutoa albamu au EP kamili kwenye WimboLink? Mwongozo huu kamili utakuelekeza kila hatua ya kuweka albamu yako. Ili kuanza kuongeza nyimbo lazima uwe na akaunti iliyowezeshwa.
Hatua ya 1: Andaa Albamu Yako
Kusanya nyimbo zako zote, jalada la albamu, na taarifa za albamu kabla ya kuanza. Hakikisha kila wimbo una kichwa wazi na umewekwa alama ipasavyo.
Hatua ya 2: Ingia kwenye Akaunti Yako ya Msanii
Fikia dashibodi yako ya msanii. Ikiwa huna akaunti, jisajili na ukamilisha uthibitisho wa msanii wako kwanza.
Hatua ya 3: Anzisha Albamu Mpya
Kutoka kwenye dashibodi yako, bofya "Albamu Zangu" kisha chagua "Unda Albamu Mpya" kuanza.
Hatua ya 4: Jaza Taarifa za Albamu
Weka jina la albamu yako, maelezo, tarehe ya kutolewa, na bei. Chagua kati ya Albamu (nyimbo 7+) au EP (nyimbo 1-6). Bei ya chini ni **TZS 2,000**.
Hatua ya 5: Weka Jalada la Albamu
Jalada lako la albamu lazima liwe **800×800** px katika muundo wa JPEG au PNG. Ukubwa wa faili usizidi **1MB**. Tumia kifaa chetu kwenye link cha kubadilisha ukubwa wa picha ikiwa picha yako inahitaji kurekebishwa.
Hatua ya 6: Ongeza Nyimbo kwenye Albamu Yako
Bofya "Ongeza Wimbo Mwingine" ili kuongeza kila wimbo chini ya mwezake. Kwa kila wimbo unahitaji:
- Weka jina la wimbo
- Weka faili ya sauti/video (hadi **200MB** kwa wimbo)
- Weka maneno ya wimbo (hiari)
- Weka wasanii walioshirikishwa (hiari)
Hatua ya 7: Kagua na Chapisha
Kagua nyimbo zako zote, maelezo ya albamu, na mipangilio. Kila kitu kinapoonekana sawa, bofya "Chapisha Albamu."